True Christianity
True Christianity - An Online Christian Community and Christian Forum
But he that hates his brother is in darkness, and walks in darkness, and does not know where he walks, because the darkness has blinded his eyes. 1 John 2:11
Home :: Teachings :: Forum :: Newsletter :: Christian Family Ministries :: Message Board :: Contact :: Call Toll Free 1(888)367-6774
Home of the Body of Christ
UONGOZI WA KIUNGU 08/10/06
UONGOZI WA KIUNGU

KUITIMU NA KUTOITIMU
Hili ni toleo la kwanza katika muandamano wa mafunzo ya bibilia kuhusu uongozi wa kiungu katika mwili wa Kristo.
Wakati ni mfupi – ni wakati wa kanisa yote kufichwa “sarakasi”jinsi ilivyo- haya “matendo ya wanadamu” lazima yafichhuliwe waziwazi ili watu wa Mungu wachague ni nani watakayemfuata, Mungu au mwanadamu.
Lazima tuwe na uongozi kamili wa Kimungu katika Mwili wa Kristo ikiwa tutaweza kupata yote ambayo Mungu anakusudia kuachilia duniani leo.
“Si kwa nguvu wala kwa uwezo, bali kwa Roho Mtakatifu asema Bwana.

MAONO NA NENO
Mwaka wa 1976 Mungu alinenea kwamba siku inakaribia upesi. Tutakapowaona watu katika mimbara wale wanaopotosha, chafua, najisi na wanaotumia neon la Mungu kwa ajili ya mapato yao wenyewe, au kwa makusudi yasiombatana na neon la Mungu wa hukumu.

Ni ombi langu kwamba kitabu hiki kitawasababishia wale wanaoelekea pande hiyo kuwa mtazamo pande hiyo mtazamo mwingine mpya katika maisha yao na hata huduma zao na KUTUBU na KUGHAIRI ili wasije wakapotosha na kuchafua watu wa Mungu na kwamba waweze kuokolewa kutokana na mkono huu wa hukumu ya Mngu. Siku ya hukumu ya Mungu imetufikilia, kwa sababu huduma zilizoonekana kubwa zimeanza kuzimia polepole. Ninaamini jambo tunalobakia kuliona sasa ni kule kuanguka na kufa mara moja katika mambara katika Runinga, Radio na Makanisani.

Kwa vyovyote watu wengi watajitilia jukumu la kuongoza watu wa Mungu pasipokuwa na ufahamu dhabitiwa neno la Mungu na jukumu kubwa tunalowekewa nalo. Ni wazi kwamba kwa njia ingine hata “huduma” zimepoteza hofu kuu kwa kumcha Mungu ambalo watu wa Mungu wanafaa kuwa nalo.
(Methali 8:13;19-27 na 16: 6) wakati umefika kwa sisi tunaojiekelea uongozi katika kanisa la Mungu ambao ni mwili wa Kristo na kujitayarisha kwa ajili ya hukumu ya Mungu. Jinsi neno la Mungu lisemavyo hukumu inaanza nyumbani mwa Mungu. Ikiwa hatuwezi kutapanga maisha yetu na huduma ili tukafikie kiwango cha neno la Mungu. Basi lile la maana tunalofaa kulifanya na pia katika mwili wa Kristo ni kujiuzulu, tuondoke katika njia na tuache mwingine AMBAYE amehitimu kuchukua mahali pa uongizi.

Tabia za kuongoza kanisa la Mungu zinapatikana wasiwasi katika Bibilia. Kuna sehemu mbili nitakazozungumzia katika somo hili, sifa za kutenda huduma jinsi zinavyopatikana katika 1 Timotheo 3:2-7 na Tito 1:6-9 na mambo yanayoondoa sifa hizo katika huduma jinsi yanavyopatikana katika mambo ya Walawi21:16-23

MAHALI MAALUM
Kwanza ningependa ni kuelekeze mahali ambapo Mungu ataiweka huduma yake iendelee. Lolote ninaloweza kupata katika neno la Mungu kuhusu somo hili ni kwamba Mungu anapenda huduma yake itendeke katika KANISA HURU LA KINYUMBANI. Siwezi kupata mahali popote katika neno la Mungu likizungumzia kuhusu “Vikundi kubwa za Makanisa” “para-church”, mahuduma za watu, shule za Bibilia, dhehemu za wanadamu ama ata zingine ambazo zimechipuka hivi majuzi ambazo huitwa “Mitembeo ya kiutume. Ndio mimi naamini katika mwito mitume lakini sio katika hili jipya ambalo ni dhehebu lisili na jina. Pata kusoma kutoka kwenye kitabu chetu kitwacho “Tabaka tano za Huduma” ninaweza kupata kanisa la kinyumbani likiimarisha watu katika Neno la Mungu (Kanisa la kinyumbani ndilo shule ya Bibilia katika chaguo la Mungu). Kisha likiwatuma kutoka katika KANISA LA KINYUMBANI kwenda kupanda, kujenga na kuyasaidia makanisa mengine ya kinyumbani kutenda kazi ya huduma. Hizi “huduma” zilizo kando na maandiko Matakatifu zimepotosha watu wa Mungu na kuzipulizia mbali pesa za Kanisa la Kinyumbani kwa muda wa kutosha. Ni wakati sasa msimamo uwekwe kinyume na huduma hizi za uwongo zinazoondolea watu wa Mungu mbali na kanisa la kinyumbani mahali ambapo wanaweza kutakaziwa, kuumbiwa, kulainishwa na kulelewa. Siku la KANISA LA KINYUMBANI limefika. Mungu anatembea katika kanisa la kinyumbani kuliko wakati mwimgine wowote. Ni HAPA TU ambalo huduma kamili ya Mungu kwa watu wake inaweza kutendeka. Siongei kuhusu mjengo Fulani, ama mjengo wa aina Fulani bali ni kusanyiko la mwili wa wanaoamini ambao wanaongozwa na mpangilio wa Mungu watiwe mafuta ya Mungu na watu wanaoongozwa na Roho. Haihitajiki uwe na mjengo Fulani lakini vyema ukiwa nao unaweza kukutania katika hema Fulani. Mnaweza kupangisha nyumba, chumba cha kupangisha nyumbani kwa mtu haijarishi mtakutania wapi, kanisa ni watu. Jambo muhimu ni kwamba mnakutana kama kanisa la agano jipyaambalo limeitwa na linaloongozwa na Roho wa Mungu sasa na tutazame tabia ama sifa za viongozi hawa wa kanisa hili la kinyumbani na mambo yale yatakayo muondolea sifa kiongozi yeyote anayeonekana kana kwamba anaweza kuongoza












TABIA ZA KUONGOZA KULINGANA NA 1 TIMOTHEO 3:2-7
Tutakuwa tunayatazama maneno ya kigiralia au kiyunani ambayo yametafusiriwa, pia jinsi maandiko matakatifu yametafusiriwa. Tutaanza na kutazama tafsiri ya Amplified, ambayo imejaribu sana kueleza tabia hizi. “Basi imempasa askofu (Mzee kanisa) (msimamizi mwangalizi) awe mtu asielaumika, mume wa mke mmoja mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, (lazima awe) mkaribishaji, ajuaye kufundisha, si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; (akionyesha upendo na kuwa na waumini wengi zaidi sana kwa wageni na wapitaji bali awe mtu mpole si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mtu wa kupenda fedha. Mwenye kuisimamia nyumba yake ajuaye kulisha watoto wake katika ustalivu (yaani asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe atalitunza kanisa la Mungu) Wala asiye mtu aliyeongoka karibu asije akajivuna akaanguka katika hukumu la Ibilisi. Tena inampasa kushuhudiwa mema na watu walio nje ili asianguke katika laana na mtego wa Ibilisi.
LAZIMA HAWE
Asipatikane na lawama – 423-Anepileptos bila lawama asiweze kukemewa. Mzee kanisa lazima awe na maisha ya kiuzee (sehemu zote) ili pasiwe na mtu au yeyote kuweza kupigana naye, kumkosoa, kumchanganya au kukosa kumtii kwa sababu ya ila katika maisha ya kiuzee. Mzee wa kanisa (hata zaidi ya wakristo wengine) hana maisha yake binafsi au maisha yake ya kiulimwengu. Maisha yake yote yametiishwa katika sheria za kikristo.
Awe mume wa mke MMOJA – mume – 435 Aner mtu mme mmoja. Mke – 1135 – Gune – mwanamke, mke. Tafsiri mingi zimepeanwa katika sifa hii, bali moja tu hupatikana katika hali sahihi ya neno la Mungu. Lazima awe na mke mmoja pekee, hawezi kuwa na zaidi ya mke mmoja kulingana na sheria. Tukisoma maandiko tunapata ya kuwa anapaswa kuwa na mke mmoja yaani yule aliyekuwa naye siku ya kuokoka au ikiwa hakuwa amefunga ndoa wakati wa kuokoka awe ni yule aliyemuoa tangu alipookoka. Tofauti tu ni wakati mke wake alikuwa haamini na ameamua kumuacha katika hali ya maandiko inasema yuko huru kufunga ndoa na mwingine. Anahitajika awe mume wa mke mmoja tangu wakati alipookoka. Soma Waefeso 6
Kinyume na mafunzo ya watu wengine Bibilia haimpigi mtu ambaye atalakiwa kwa sababu ya kuokoka kwake. Kulingana na Bibilia mtu akibadilika awe mkristo mambo ya kale huwa yamepita; tazama yote yamekuwa mapya. Hii ina maana kwamba ya kale yamesamehewa na Mungu akisamehe huwa ni kana kwamba haikuwepo au haikutendeka kwa hivyo haiwezwkani mtu akapigwa na mambo hayo.
Hawe mwangalifu tu – 3524 – Nephaleos – kiasi awe na busara, hawe mwenye kiasi – 4998 – sophron awe mzima mwenye akili zilizojaa busara, utu wema, mwenya namusi mwema, mwenye uaminifu kiasi, mwenye tabia za kujiweza. Maisha yake lazima yawe yameimarika au yana dalili za kuimarika.
Lazima awe mwenya akili zenye hekima, akiwa ana upangilio wa maisha yake vyema na hata katika neno la Mungu. Asiwe mtu wa kupayukapayuka maneno ila atakuwa akishikilia habari kwa siri ambazo zinaweza kuleta utata zikifichuliwa.
Awe na tabia njema – njema- 2579 – Kalos - njema, bora ya dhamana, yastahili, njema zaidi, adilifu, Tabia – 2887 – Kosmios – taratibu, adabu ya tabia njema yenye kiasi anapoonekana. Yampasa aelewe kwamba yeye si wa tabia “zuri ya kipekee mno” bali aelewe ya kuwa yeye ni mfano mwema kwa watu wa Mungu hivyo basi yeye bila kusita lazima awe na tabia inayomuiga Kristo kila wakati.
Awe mkaribishaji – 5382 – philoxenos – mpenda wageni, mkaribishaji, amejitolea/upendo ukarimu; anayependa watu wa Mungu na kufurahia ushirika wao. Lazima awapende wakikaa nyumbani mwake pengine wanaweza kuwa na taji.
Awe tayari kufunza 1317 – Didaktikos – kuelekeza, tayari kufunza, hodari na umaarufu wa kufunza. Lazima awe tayari kufunza kwa njia ambayo yeyote anayemskiliza anaelewa. Mabadiliko yanayotokea katika watu anayewafunza yanafaa kumchochea kuendelea kufunza zaidi.
Lazima asiwe mlevi – 3943 – paroinos – kukaa karibu na pombe, mtu mlevi, anayelewa. Pombe isiwe tabia /kanuni maishani mwake. Elewa, maandiko hayasemi (wengine wengi hawaelewi) kwamba huwezi kunywa mvinyo inasema asiwe mlevi. Lazima atawale mambo yote maishani mwake, asitawaliwe nazo.
Asiwe mwenye ubishi – 4131 – plektes – mwenye mabishano, mwenye ugomvi, fujo, mpiganaji (wakupigana). Asiwe mwepesi wa hasira ama mwenye kukasirika haraka na kuanza vita. Asiwe anaweza kulawa na yeyote ili apatwe na hasira na kuanza kubishana.
Asiwe mwenye tamaa ya mali – 146 – Alschrokeroes bila tama, mwenye kutamani mali sana, asiwe na uchoyo
Chafu – Aischrolagia – matamshi machafu, matamshi yenye kukwasa, asiwe anaweza kupotoshwa na pesa. Asiwe anaweza kuwa anatawaliwa na pesa katika kufanya uhamisi au matendo yake.

Awe mwenye uvumilivu – Epielkes – jitwalia, asiwe mkali, mpole, mwenye kiasi, mvumilivu, mwenye haki awe mwadilifu. Uvumilifu ni tabia inayofaa kuwa imejaa maisha yake yote

Asiwe wa kuleta ghasia – 269 – amachos – wa kuweka amani, si wa ugomvi, hajiruhusu, aweza kuingizwa katika hali ugomvi au ghasia

Asiwe wa kutamani – 866 – Aphilarguros – bila tama. Lazima asiwe na tamaa yeyote ile ambayo imeshinda kupenda Roho wa Mungu na upako wake.

Awe anatawala nyumba yake vyema – kutawala 4291 – Proistemi – kiongozi mtawala, juu anasimamia nyumba – 3624 – Oikos – jamii, boma, makao. Lazima awe kiongozi wa nyumba yake. Asitawale kinyume na maandiko matakatifu bali awe anapokea heshima zake kama mtu wa Mungu na kichwa cha nyumba yake.

Asiwe mpya katika wokofu – 3504 – Neophlitos – mpya, mchanga katika imani, amepadwa majusi. Anatakiwa kuwa mwalimu aliyehudumu katika maandiko kwa muda mrefu zaidi ili awe na ufahamu wa neno la Mungu. Lazima awe amefikia kiwango Fulani cha ukomafu ambao una tabia zinazoambatana na mwito wa kiuzee wa kanisa.

Imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje – mema – 2570 – Kalos – mema, inayostahili njema. Habari – 3141 – Marturia – Habari shuhuda, ripoti, ushhuhuda habari iliyotolewa. Bila – 1855 – Exothen – iliyotolewa humo nje huko. Maisha anayoyaishi akiwa kanisani lazima yawe sababa na yale anayoyaishi akiwa nje ya kanisa. Wote wanaomjua lazima wasiwe na nafasi yoyote ya mashtaka ya haki kwake.

TABIA ZIZIZOSTAHILI
Katika agano la kale, mambo ya walawi 21:16-23 kuna dosari zile za kimwili ambazo tunaziona zinazomzuiya mtu kuifanya kazi ya ofisi ya kuhani hata kama alikuwa ameitwa kuifanya. Kwa maneno mengine wale waliokuwa na ila hizi hata kama walikuwa wamezaliwa katika jamii ya kikuhani , hawangeweza kuhudumu mbele za Mungu na mbele za watu wa Mungu. Bali yeye yu ngali wa jamii ya kikuhani. Angalikuwa “ameokoka” na kushiriki vita vitakatifu au kula vitu vitakatifu. Angalifurahia faida ya kuwa katika jamii ya kikuhani, BALI alikuwa hawezi kuhudumu. Angaliweza kuwa kuhani (mhuduma), hangaliweza KUMWAKILISHA Mungu kwa watu. Au asimame mbele za Mungu kwa ajili ya watu. Ikiwa ukuhani wa Agano la kale uliomfanya mtu kuwa kuhani kwa kuzaliwa katika jamii ya familia ya makuhani ulikuwa na tabia za kumwondoa mtu asiwe kuhani, yawezekanaje sisi tuliye “chaguliwa tu” tujidhanie kwamba twaweza kufanya mambo kivyetu na tusiweze kutubu na kubadilisha mambo katika maisha yetu yasiyompendeza Mungu au tuondolewe.

Kwa sababu Agano la kale hunena kwa ishara na mifano na maandiko matakatifu yanasema kwanza la kawaida la Rohoni, hebu tutazame tabia zizizostahili katika Agano la kale katika hali ya kiroho. Jinsi zote tujuavyo hali ya ulema, kwa sasa haiwezi kuzuiya mtu kuwa kuhani, bali ulema wa rohoni utamfanya mtu kutokubaliwa kusimama mbele za Mungu na watu wake.

Mambo ya Walawi 21:5-8, 17-23. NKJ (KJV) “wasijifanyie upaa kichwani wala wasinyoe pembe za ndevu zao, wala wasichaje chale katika miili yao. Watakuwa watakatifu kwa Mungu wao wala wasilinajisi jina la Mungu wao, kwa kuwa wao ndio wasongezao sadaka za Bwana kwa njia ya moto, chakula cha Mungu wao; kwa ajili ya hao watakuwa watakatifu, wasimuoe mwanamke aliye kahaba, au huyo aliye mwenye unajisi, wala wasimuoe mwanamke aliyeachwa na mumewe kwa kuwa yeye kuhani ni mtakatifu kwa Mungu wake. Kwa hivyo basi utamtakasa, kwa kuwa yeye husongeza chalula cha Mungu wako; atakuwa mtakatifu kwako wewe; kwa kuwa mimi bwana niwatakasaye ninyi ni mtakatifu.
“Nena na Haruni umwambie mtu awaye yote wa kizazi chako wewe katika vizazi vyao, aliye na kilema, asikaribie kuongeza chakula cha Mungu wake. Kwa kuwa mtu awaye yote aliye na kilema hatakaribia; mtu kipofu au kiwete au mtu aliye na pua iliyoharibika au aliye na kitu kilichosidi ipasavyo mwili au mtu aliyevunjika mguu mguu au mkono, au aliye na kijongo au aliye kibeti au aliye na kilema cha jichoni au aliye na upele au mwenye buba au aliyevunjika mapumbu ; mtu awaye yote wa kizazi cha Haruni kuhani aliye na kilema huyo asikaribie kusongeza chakula cha Mungu wake. Atakula chakula cha Mungu wake katika hicho kilicho takatifu sana na hicho, na hicho kilicho takatifu lakini hataingia ndani ya pazia wala asikaribie madhahabu kwa sababu ana kilema; ili kwamba asipanajisi patakatifu pangu; kwa kuwa mimi ndimi Bwana niwatakasaye.




LAZIMA ASITUMIKIE MIUNGU YA UONGO
Kunyoa pembe za ndevu kufanya upaa katika kichwa “kumimina damu” kukata mwili yote ilikuwa ni ishara ya kuabudu miungu. Kwa maneno mengine mtu wa Mungu ni lazima awe mwangalifu sana ili asiyafuate matendo ambayo maana yake haswa ni kuabudu miungu ya uongo. Mfano wa ili yawezekana kuwa “The Easter Sunrise Service” au kuifanyia baada ya jua linapochomoka upande wa mashariki, tabia ambayo madhehebu huifanya na kuifauata, bali hiyo kiini chake kimetokana na kuabudu mungu wa uongo wa Misri anayeitwa Ra [Mungu wa jua wa Misri]
LAZIMA AFUNGE NDOA SAFI
Mtu a Mungu kwanza ameoana na Mungu, pili na mke wake.Hawezi kuchanganya kitakatifu na kinajizi,si mnajisi.Hawezi kuwa sehemu ya maisha ya kuhaniwa Mungu.Mtu aliye kuhani wa Mungu hawezi kuwa na na mafunzo mengine isipokuwa yale yanayo patikana katika bilbilia takatifuya Mungu na hawezi kuchanganya kichafu na kitakatifu.uhusiano wake na neno la Mungu.[mungu]wapaswa kuwa kama wa wake na wa mke wake,hadi kifo kitutenganishe, lazima awe mtiifu kwa Mungu wala asiende kando halo awe aanapenda lisemwalo au la.hawezi kuliongezea au kulifunguza.lazzima ayalinde maisha yake, mafundisho yake, kuelewa kwake, chochote asemayo, afanyacho na kiwa sababu kwa neno lo Mungu.

MTU KIPOFU
Wakati mtu aliye kipofu wa macho hajakatzwa kuwa mhudumu. Mtu aliye kipofu wa roho hafai kuwa muhudumawa watoto wa Mungu.bahati mbaya wengi ambao ni vipofu rohoni huendelea (hujaribu) kulisha watu wa Mungu,wakiwaletea magonjwa ,kuchanganyikiwa, upotofu na hukumu ya milele.mtu kipofu pamoja na marafiki zake huwaletea watu kile ambacho wamekiona na faida kwao, hufunza maandiko yale ambayo huwaletea pesa zaidi hupenda halaiki la watu ili wajipatie pesa, hupenda wakati wanapo tembea huku na kule akijidai wanahubiri sanaupenda sana ilietabia ya kuvutwa kwa urahisi kwa myoto ya “charima” isiyo na roho mtakatifu ndani yake iliwapate chocote wanachotaka. Hata anawezaa kutumia sarakasi za kitamaduni akikubaliana na maagizo ya wale wanaoamini kuliko neno a Mungu, badala ya ujifunza na kumuomba Mungu ili ampe muelekeo kamili la neno la Mungu.tafsiri ningi za Bibilia zingine HAZIAMBATANI NA MAANDIKO TAKATIFU ila mtu ambaye ni kipofu wa rohoni hawezi kuelewa ili.yeye hukubali na kulisha watu wa Mungu mkate uliyo tiwa chafu.wale watu anaye waongoza nao huwa vipofu pia na hapo lile kanuni la neneo la Mungu utumia, kipofu anapoongoza kipofu mwenzake wote hutumbukia shimoni. YEYE HAFAI kuhudumu hadi atakapopona, anafaa KUJIUZULU mpaka atakapo anza kuona.
MTU KILEMA.
Kilema hana uwezo wa kutembea vyema, bali haja katazqwa kuhudumu katika huduma ya kisasa. Hata hivyo klema wa rohoni, mtu anaye jidayi kwamba ni muhudumu wa Mungu, yule hawezi kutembea vyema katika utakatifu hafai kuhudumia watu wa Mungu. Yawezekana yeye ni mzima kabisa kwa nje,inawezekana ana ujuzi wa kutafsiri neno la Mungu vyema na kulielewainawezekana anaelewa kila funzo na kanuni za maamndiko, inawezekana anaweza kukuwaletea mifano na picha nzuri za yesu Kristo, kwa njia nzuri, safi,na wenye uzito kiasi kwamba watu uliyakatika mifano yake bali ikwa hawezi kuishi kwyo, ikiwa mtu wake wa rohoni hawezi kutembea katika nen hilo yeye hafai kuwa muhudumu wa watu wa Mungu.
Hata hivyo wengi huendelea na (kujaribu)kuongoza watu wa Mungu wakiwapatia mifano ya yeye ulema hhivyo bvasi wakiwapotosha zaidi.si ajabu kwamba watu wengi wa Mungu hawawezi kuishi maisha matakatifu, maisha yao yamedhohofika zaidi, hujikwa na kuanguka kivudiudi. Wao huenda kama viongozi wao, wao huwafuata viongozi wao, jinsi wanavyoelezwa, wla siyo krito.


SURA ILIYO HARIBIKA
Sura iliyo haribika inaweza kuwa na umbo nyingi.tafriri ya Yakobo inanena huhusu pua iliyo haribika, basi tuanze na sehemu hii ya sur. Sura hunena huhusu kufafanua. Pua hunusa mema na mabaya , inaweza kueleza ni lipi jema la kula, na lisilo jema la kula ila mtu aliye na pua lenye kukhaibika rohoni hawezi kutofautisha ka ti ya chakula chema na kibaya cha roho itokayo kwa Mungu na roho zinazotokana na Ibilisi.yeye atakula na ataruhusu wengine wale ambao anawaongoza, chakula kisicho faa kuliwa. Mtu aliye na pua mbaya (asiyefanya kazi)hafai kwa huduma.
Sikio ambayo ni mbaya hawezi kusukia vyema. Wakati mwingine haliwezi kusikia katukwa maana ni kiziwi.sikio la neno kuhusu kusiia.sikio lililoharibiwa haliwezi kufanya kazi vyema, linaweza kuligeuza yale ambayo linayasikia kuwa mabaya, hivyo basi lisiweze kutambua sauti linalosikia ni la nani. Linaweza kuwa sauti sote linasikia lisiweze kuzitofautisha na kuzipambanua. Linaweza lisitofautishe kati ya sauti ya Mungu nay a Ibilisi.mtu asiyeweza kusikia kabisa sauti ya bwana tayari ameharibiwakwa sababu atawapotosha wutu wa Mungu kwa sababu atafuatilia sauti zingine ambazo si za Mungu.
Mdomo uliyo haribiwa hauwezi kongea vyema, utaharibu yale uliyo ya sema kueleweka vibaya na kusababisha kuchanganyikiwa.
Mtu ambaye sura yake ya kiroho imeharibiwa ataonekana umbo mbaya mbele za Mungu naye hafai kuwa mtumishi.
KIUNGO KIREFU ZAIDI
Kiungo kirefu zaidi kinaongea juu ya sehemu moja ya mwili kuwa ndefu zaidi ya sehemu zingine za mwili.
Mtu mwenye mguu, mkono kidole nk mrefu huwa hakataliwi.bali tukitazama maana ya kiroho kuhusu hili tunaona huduma nyingi sana ambazo zinakuwa tu sehemu moja ziko nje ya umbo kamili, huwa zinafunza sehemu moja tu ya injili na kuachilia zile sehemu zingine.mfano wa hii ni ule mtembeo wa “imani” ambayo imeachilia sehemu zingine za injili pia ni za maana sana ili zikaweze kufutia sana, funzo ili la “Imani”amayo inaonekana kama mguu nadani ya kawida.
Neno la kiibrania ambalo linatumika hapa linawezekana kuwa ni kiungo kirefu zaidi ya zingine.mfano vidole sita nk. Kwa maneno mengine ni kwamba kuna kiungo kimoja zaidi ya kawaida.mhubiri aliye na kiungo zaidi ni yule anayeongezea aukutoa jambo katika neno ambalo haliko katika neno la Mungu anaharibu kweli mara kwa mara.kama katika mtembeo wa karisma wakongeza kitu huwafanya watu kukaa hoe hae inachochea mtu wa mwili ndani yao lakini si la kawaida (yaani si kimaandiko)ni kitu/jambo ambalo limeongezakiungo zaid, kitu ambacho si cha Mungu. Maandiko inasema kwamba “ mtu yeyote akiongeza maandiko atalaaniwa” anaye kiungo kimoja kirefu ama anaye zidisha ataondolewa.
MGUU ULIO VUNJIKA
Mkono unanena kuhusu neno la Mungu duniani. Mtu mwenye mkono uliovunjika hawezi kushikilia neno la Mungu vilivyo. Hawezi kwa unyovukuyashikilia na kutatua mambo ya wale walio na mahitaji kwa sababu ya mkono wke wenye maumivu. Hawezi kutenda kazi vyema kikombe na mkate kwa sababu hataweza kuchukua mkate na kushiriki au kikombe cha divai na kukipitisha katika ushirika.utumishi wake wakati wake mwingi akiulinda mkono wake sana badala ya kutumia wakati huo kulinda wale anaowahudumia.mkono uliovunjika utakaa nyuma na kufa ganzi huku ukiogopa kufaya kazi iliusije ukaumia tena.yeye nashindwa kujivakisha nguo hivyo basi atawezaje kuwavalisha wana wa Mungu? Mtu aliye vunjika mkonoatakuwa akitaka atumikiwebadala ya kuwa mtumishi akiyeitwa na Mungu. Kuwa yeye hafai.;





MGONGO WENYE KINUNDU
Mgongo wenye kinundu umeadhiriwa kwenye uti wa mgongo. Tabia zake sio nzuri, zimeadhirika. Hawezi kusimama vyema. Hawezi akafanya mambo ya injili ya Mungu vile ilivyo ila atayabadilisha yawe kombo kama yeye mwenyewe alivyo. Kwa sababu msimamo wake umeharibiwa hataweza kusimama sababa na kanuni za Mungu. Huwa atachukua msimamo mbaya katika yote anayofanya, anajihusisha na mafunzo mabaya anayoyaita “ufunuo mpya wa kisasa”, hubadilika kila wakati kama vile nyakati za “ufunuo” huu zinavyobadilika. Mafunzo yake ni kama msimamo wake ulioadhirika, hawezi kuurekebisha, hubadilika kutoka kwenya funzo moja hadi lingine. Yeye hafai aidha.

MBILIKIMO/KIDURANGO
Mtu mbilikimo au kidurango ni yule aliyekomaa ila ni wa kimo cha kiberiti. Hakufanikiwa kukua kabisa, mwili wake ulimuondokea. Hatima za mwili wake huonekana kana mtu tu, bali tunapotazama katika umbilikimo wake wa kiroho tunaona mtu aliyeacha kukua na kukosa kufikia wote ni mkristo asiyekomaa, hawezi kula mifupa ya kiroho. Hawezi kula chakula kigumu. Tumbo lake linatosheleshwa na maziwa tu. Ameacha kukua, je anawezajekuwakamilisha wateule katika hali ya ukomafu? Mtu huyu hafai katu.

JICHO LILILO NA ILA (LENYE DOSARI)
Sio kama kipofu bali huyu mtu ana uwezo wa kuona – jambo ni kwamba hawezi kuona vyema. Ana shida la boni la jicho. Anaona mambo ya Mungu kama kiwiliwili. Anaona vitu mbili kwa moja, ana shida ya kutofautisha rangi mbalimbali. Hana ufahamu wa kidani kabisa, anaona lakini sio dhairi. Huyu mhuduma anaona vitu nyingi sana; lakini anaziona zote katika mtazamo ulioharibika. Hawezi kushiriki mambo ya Mungu vyema kwa sababu mtazamo wake umeadhiriwa tayari. Kwa sababu anaona kwamba anajaribu kuwashawishi watu ili wamuelewe hapo anaanza kuwakaganya, kuwaelezea picha zilizo kombo, anaweza kufunza kile anachoona, yaani picha zilizoadhiriwa. Mtu kama huyu hafai kamwe.

MTU MWENYE KISEYEYE (SCURVY)
Ugonjwa wa kuvimba kiseyeye husababishwa na ukosefu wa madini au vitamini C mwilini, mtu asipokula vyakula vinavyotakikana kwa kuipata vitamini C hugonjeka ugonjwa wa kiseyeye (scurvy). Vyakula mbichi kila wakati zimejaa vitamini C na madini nyingi, vyakula kamili vitapea mtu vitamini C ya kutosha na hivyo basi kuzuia ugonjwa huu wa kiseyeye (Scurvy). Mtu mwenye ugonjwa huu wa kiseyeye huwa anakula chakula cha kale, kwa maneno ya kiroho ni aina ya mhuduma ambaye tegemeo kale ni kusoma vitabu vya zamani, mahubiri ya zamani, masomo ya zamani, kuelewa kwake ni kule kwa zamani. Huyu mtu mwenye ugonjwa wa kiroho wa kiseyeye huwa hamruhusu Mungu kumfunulia ufunuo mpya, katika wingi wa maarifa ya neno la Mungu. Yeye huogopa kula chakula kibichi cha neno la Mungu kwa maana hajui chatoka wapi. Huwa hawezi kumsikia Mungu wala kuelewa maandiko matakatifu ya Mungu kwa hivyo hukataa kula chakula mbichi cha neno la Mungu. Ni mara ngapi unasoma neno la Mungu mahali ambapo unapajua na wakati huo Mungu anakupa ufunuo mpya na kuielewa iliyoandikwa vyema zaidi. Hili haliondoi kitu chochote kuhusu maarifa yako ya kuelewa andiko hilo la zamani, bali linakuongezea ufahamu zaidi na hivyo basi kuwa na vitamini C zaidi katika maisha yako ya kiroho, ukijiweka katika afya njema ya kiroho na katika mtembeo sababa na Mungu. Huyu mtu mwenye ugonjwa wa kiseyeye huwa na madhara mengine mengi yanayomfanya kuendelea kula chakula cha zamani na kumkosesha kusikia sauti ya Mungu wake. Mtu kama huyu hafai hata kamwe.
MTU MWENYE UPELE
Upele wa kiroho unapatikana katika Timotheo wa pili 4:3 “kwa kuwa wakati utafika watu hawatafumilia kusikia habari kamili za Mungu, bali wakiwa na masio yenye kiwasho (kwa mambo matamu matamu wanayojitakia) watajikusanyishia wenyew wahubiri wanaojitakia wenyewe ili wawahubirie yale wanayotaka kusikia wenyewe watageuka na kulikataa kweli na kuanzisha ekaya na hadithi za binadamu, mtu mwenye upele
PAPER H
Atakuwa kila mara akitafuta “ufunuo mpya”, mafunzo mapya, mafunzo yanayopendeza nafsi yake mwenyewe yanayokubaliana naye bila kujali kile neno la Mungu husema. Atawapotosha watu wa Mungu, mtu kama huyu hafai.

KIGAGA
Vindoda vyenye kutunga usaha vinaeleza kibaga ubaga kuhusu hali hii ya kutofaulu kama mhuduma. Kindoda kinachotunga usaha kimeoza na hakiwezi kupona. Hukaa kikijifunafuna mara kwa mara. Hili linaongea kuhusu uchungu moyoni na kukosa msamaha, kindoda ambacho hakijalindwa vyema ili kiweze kupona , kindoda hiki huendelea kuoza na kutunga usaha. Aina ya kukosa msamaha kama hii huleta uchungu mwingi wa moyo ambao huendelea kuozesha hicho kindoda na kukifunua ili kila mtu aweze kukiona. Mtu akiwa na ugonjwa wa kiroho kama huu kila mara huhudumia watu neno kali a kwa uchungu. Mtu kama huyu hafai hata kamwe kuhudumu.

NGOZI INAYOSUMBUA
Ngozi ikisumbua huwa ina upele na mara kwa mara vindoda huchipuka ndani yake, hufanya mtu kukosa kutulia. Huwa ana wasiwasi na hawezi kukaa na kuweza kutulia na kuwasikiza wengine. Mtu kama huyu hunena habari zake kisha anaamka na kwenda. Hana wakati wa kusikiliza wengine hupenda kusimulia wengine habari zake tu na anaamka na kwenda zake. Kuwaa anajishughulisha na upele wake mwenyewe na hana wakati wa kusikiliza wengine kwamba wamefika wapi. Hajali wengine kwanza. Mtu huyu hafai.


MTU TOWASHI/MHASI
Mtu towashi ni yule mwanamume asiye na uwezo wa kupata au kuzalisha watoto. Hali yake ya mwanaume imeharibiwa. Tuangalie sasa hali ya kiroho ina maana gain. Huyu ni aina ya mhubiri ambaye hawezi kulileta neno la Mungu jinsi lilivyo. Watu wanapomsikiza na kumfuata hawawezi kupata maisha mapya na kubadilika. Wahubiri wengi wanaweza kuhubiri injili kwa msisimko mwingi, wanaweza kuhubiri kuhusu yesu, ila hawahubiri kwa nguvu zinazoweza kubadilisha maisha kwa sababu hawamjui na hawaamini anaweza kubadilisha maisha ya watu. Wanajua kumhusu ila hawamjui. Hawana nguvu za kumhubiri Yesu pasipo kukubaliana, usafi, kweli na bila ila kwa sababu hawatembei naye. Hali yao ya uzazi wa kiroho imeharibiwa, haiwezi kuleta maisha. Hawafai hata katu.

TUMAINI KWA WOTE

Funzo hili halifai kuleta kufa moyo kwa yeyote, ila limepangwa kuyafungua macho ya watu wale walioitwa kuongoza wengine na kupewa jukumu ya kufunza neno la Mungu.
Je una baadhi ya dosari hizi?
Funzo hili halimaanishi kufungua macho ya wanadamu wanaohusika kuongoza na kufunza watu wa Mungu.
Je una baadhi ya dosari hizi?
Kama unazo ni rahisi kurekebisha enda kwa Mungu TUBU, BADILIKA halafu endelea. Kunao wapendwa wengi katika HUDUMA hawahitimu kwa vitu vya kiroho.
Ni wakati wapendwa hawa kutubu na kubadilika kabla Mungu hajaleta hukumu juu yao. Kama wewe ni mmoja wa wale hawaitimu tubu na ubadilike ama “USHUKE CHINI|”. Itasaidia maisha yako kama unafanya kazi kulingana na njia za Mungu lazima anaendelea na kukubariki. Fikia wale bado na uwasaidie kupata njia ya kweli Wagalatia 6:1
Ndugu zangu kama mtu akipatikana katika kosa lolote ninyi mnaoongozwa na Roho Mtakatifu wa Mungu mumwonye mtu yule katika njia safi, mkimrudisha kwa roho ya upole na kujiangalia kusudi asijaribiwe mwenyewe 22:9

Mariko 16: 17 – 20
Wanaoamini watafanya maajabu haya:
Watafukuza mashetani kwa jina langu,
Watasema kwa lugha mpya , wakishika nyoka au kunywa sumu yoyote hawatakufa.
Wataweka mikono yao juu ya wagonjwa nao watapona.
Alipokwisha kusema nao hivi, Bwana Yesu akachukuliwa juu mbinguni akaketi upande wa kuume wa Mungu.
Wanafunzi wakaenda kuhubiri popote. Bwana akatumika pamoja nao na kuhakikisha ukweli wa mahubiri yao kwa maajabu waliofanya.
Amen.
 Kama ishara zimetajwa juu haziambatani nawe unapohudumia wadugu lazima ujichunguze na baba yako na utafute kwa nini haziambatani nawe.
 Hii sio wadugu Fulani lakini kwa kila mkristo sana sana kwa wanaoongoza watu wa Mungu.
 Tubu kuwa laini na Mungu (ondoa mambo ambayo hayafai maishani mwako kasha “maajabu haya yatakufuata”
 Mungu akubariki anapomfuata

Charles Lafoe
Baadhi ya vifaa vya kuhitimu vimepatikana kutoka kitabu cha backbones, scurvy and broken stones by Bill Britton
- Hiki kitabu kinapatikana kwa huduma yetu pia.
- Vitabu vya mafunzo haya na vingine vinapatikana kutoka kwa anwani zilizo hapa chini. Hatuna cha kuuza. Chochote tunacho kinatokana na Mungu ni chake.
Christian Family Ministries

Christian Family Ministries
34 Martin Ln
Fair Grove MO 65648
USA
417 – 860-1180

KENYA ADDRESS
P.O. BOX 4969 - 00200
CITY SQUARE
Tazama katika mtandao wetu
NAIROBI - KENYA
EAST AFRICA

http://www.truechristianity.org

VITABU/BOOKS
MAMLAKA YA NYUMBA YA KIKRISTO
VILIVYOBAINISHWA
- MWANDAMO WA MAFUNZO YA ROHO MTAKATIFU
1. MAFUNZO YA UPUMBAVU
2. JE, KAZI YA MHUDUMU NI GANI
3. MUNGU ANATAKA UWE NA TABIA
- MWANDAMO WA MAFUNZO YA UONGOZI
1. UONGOZI WA KIUNGU
MWANDAMO WA KWELI ZA MAANDIKO
MWANDAMO WA DOKEZO LA MAFUNZO
TEPE/KANDA ZA MAFUNZO
- Orodha za mafunzo hayo zipo.
HUDUMA ZA KUSAFIRI
• MAFUNDISHO
• MAHUBIRI
• UNABII
Tunaendelea kuongeza orodha iliyopo hapo juu.
Kwa taarifa zaidi tuandikie au utazame kwenye mtandao wetu.
http://www.truechristianity.org



Bible Keyword Search
Search BibleGateway.com
© 2007 Christian Family Ministries